Uzi malumu kwa ajili ya Jumapili kanisani

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,915
Reaction score
4,062
Points
2,100
Bwana Yesu Asifiwe?
Tumsifu Yesu Kristo?
Mwana kondoo ameshinda!
Shalom shalom!
Najua mko poa kabsaa, lengo la uzi huu ni kucomment somo ulilojifunza siku ya juma pili, kama hunapata shida kuandika unapost tu neno pekeake bila maelezo, hivyo yani kwanzia kesho natarajia mtatuma ili tujifunze wote.. karibu na Asante uzidi kubarikiwa
 
Gily

KF Founder & Dragon IGM
KF Founder
Joined
Jun 4, 2023
Messages
8,338
Reaction score
31,699
Points
2,100
KATOLIKI - MASOMO YA MISA, JUMAPILI, SEPTEMBA 24, 2023
JUMA LA 25 LA MWAKA

MWANZO
YbS 36:15.16

Bwana asema: Mimi ni wokovu wa watu. Wakinililia katika taabu yoyote nitawasikiliza, nami nitakuwa Bwana wao milele.

SOMO I
Isa. 55:6 – 9

Mtafuteni Bwana, maadamu anapatikana, Mwiteni, maadamu yu karibu; Mtu mbaya na aache njia yake, Na mtu asiye haki aache njia yake, Na mtu asiye haki aache mawazo yake; na amrudie Bwana. Naye atamrehemu; Na arejee kwa Mungu wetu, Naye atamsamehe kabisa.

Maana mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu; asema Bwana. Kwa maana kwa vile mbingu zilivyo juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko nchi, kadhalika njia zangu zi juu sana kuliko njia zenu, na mawazo yangu kuliko mawazo yenu.

Neno la Bwana...Tumshukuru Mungu

WIMBO WA KATIKATI
Zab. 145:2-3, 8-9, 17-18 (K) 18

(K) Bwana yu karibu na wote wamwitao.

Kila siku nitakuhimidi,
Nitalisifu jina lako milele na milele.
Bwana ndiye mkuu mwenye kusifiwa sana,
Wala ukuu wake hautambulikani. (K)

Bwana ana fadhili ni mwingi wa huruma,
Si mwepesi wa hasira, ni mwingi wa rehema.
Bwana ni mwema kwa watu wote;
Na rehema zake zi juu ya kazi zake zote. (K)

Bwana ni mwenye haki katika njia zake zote,
Na mwenye fadhili juu ya kazi zake zote.
Bwana yu karibu na wote wamwitao,
Wote wamwitao kwa uaminifu. (K)
________

SOMO 2
Flp. 1:20-24, 27

Kristu ataadhimishwa katika mwili wangu; ikiwa kwa maisha yangu, au ikiwa kwa mauti yangu. Kwa maana kwangu mimi kuishi ni Kristo, na kufa ni faida. Ila ikiwa kuishi katika mwili, kwangu mimi ni matunda ya kazi; basi nitakalolichagua silitambui.

Ninasongwa katikati ya mambo mawili; ninatamani kwenda zangu nikae na Kristo; maana ni vizuri Zaidi sana; bali kudumu katika mwili kwahitajiwa Zaidi kwa ajili yenu. Lakini mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo.

Neno la Bwana...Tumshukuru Mungu
________

SHANGILIO
Yn. 1:12, 14

Aleluya, aleluya,
Naye Neno alifanyika mwili, akakaa kwetu;
Wote waliompokea aliwapa uwezo wa
kufanyika watoto wa Mungu.
Aleluya.
________

INJILI
Mt. 20:1-16

Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Ufalme wa mbinguni umefanana na mtu mwenye nyumba, aliyetoka alfajiri kwenda kuajiri wakulima awapeleke katika shamba lake la mizabibu. Naye alipokwisha kupatana na wakulima kuwapa kutwa dinari, aliwapeleka katika shamba lake la mizabibu. Akatoka mnamo saa tatu, akaona wengine wamesimama sokoni wasiokuwa na kazi; na hao nao akawaambia, Enendeni nanyi katika shamba langu la mizabibu, na iliyo haki nitawapa. Wakaenda. Akatoka tena mnamo saa sita na saa kenda, akafanya vile vile. Hata kama saa kumi na moja akatoka, akakuta wengine wamesimama, akawaambia, Mbona mmesimama hapa mchana kutwa bila kazi? Wakamwambia, Kwa sababu hakuna mtu aliyetuajiri. Akawaambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu. Kulipokuchwa, yule bwana wa shamba akamwambia, enendeni nanyi katika shamba la mizabibu. Kulipokuchwa, yule bwana wa shamba akamwambia msimamizi wake, Waite wakulima, uwalipe ujira wao, ukianzia wa mwisho hata wa kwanza. Na walipokuja wale wa saa kumi na moja, walipokea kila mtu dinari. Na wale wa kwanza walipokuja, walidhani kwamba watapokea Zaidi; na hao pia wakapokea kila mtu dinari. Basi wakiisha kuipokea, wakamnung’unikia mwenye nyumba, wakisema, Hao wa mwisho wametenda kazi saa moja tu, nawe umewasawazisha na sisi tuliostahimili taabu na hari za mchana kutwa. Naye akamjibu mmoja wao, akamwambia, Rafiki, sikudhulumu; hukupatana nami kwa dinari? Chukua iliyo yako, uende zako; napenda kumpa huyu wa mwisho sawa na wewe. Si halali yangu kutumia vilivyo vyangu kama nipendavyo? Au jicho lako limekuwa ovu kwa sababu ya mimi kuwa mwema? Vivyo hivyo wa mwisho watakuwa wa kwanza, na wa kwanza watakuwa wa mwisho.

Neno la Bwana...Sifa kwako, ee Kristo
 
Safi sana
 
Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,915
Reaction score
4,062
Points
2,100
Yohana 14:1, 15-16, 25-26

Yesu akawaambia, “Msifadhaike mioyoni mwenu, mnamwamini Mungu, niaminini na mimi pia.
“Kama mnanipenda, mtazishika amri zangu. Nami nitamwomba Baba, naye atawapa Msaidizi mwingine akae nanyi milele.
“Nimewaambia mambo haya yote wakati bado niko pamoja nanyi. Lakini huyo Msaidizi, yaani, huyo Roho Mtakatifu, ambaye Baba atamtuma kwenu kwa Jina langu, atawafundisha mambo yote na kuwakumbusha yote niliyowaambia.”

Hilo ndio somo la leo kanisani kwetu.. kifupi ni kwamba kama tulivo mwamini Yesu tukampokea na kumpa maisha yetu, ndio tunatakiwa kumwamini roho mtakatifu aliye ndani yetu ili aweze kutusaidia katika kila jambo, kwa maana yeye ni mwalimu, anaweza kutufundisha yote..
 
Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,915
Reaction score
4,062
Points
2,100
1Petro 1:18-19
18 Nanyi mfahamu kwamba mlikombolewa si kwa vitu viharibikavyo, kwa fedha au dhahabu; mpate kutoka katika mwenendo wenu usiofaa mlioupokea kwa baba zenu;

19 bali kwa damu ya thamani, kama ya mwana-kondoo asiye na ila, asiye na waa, yaani, ya Kristo.

Hilo ndilo neno la leo, ni hivii sadaka ya ukombozi ni DAMU YA YESU ukiambiwa utoe hela au chochote umeliwa, kwamaana bibilia imeeleza fedha na dhahabu ni vitu viaribikavyo inapokuja kwenye suala la UKOMBOZI..
 
Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,915
Reaction score
4,062
Points
2,100
Wandugu hili ndio neno la jumapili jana kanisani kwetu.

Isaya : Mlango 45

2 Nitakwenda mbele yako, na kupasawazisha mahali palipoparuza; nitavunja vipande vipande milango ya shaba, na kukata-kata mapingo ya chuma;

3 nami nitakupa hazina za gizani, na mali zilizofichwa za mahali pa siri, upate kujua ya kuwa mimi ni BWANA, nikuitaye kwa jina lako, naam, Mungu wa Israeli.

Tulijifunza kuwa kuna hazina na mali ziko gizani, ambazo ni stahiki yetu, na moja kati ya njia ya kuzipata ni "kutoa". Utoaji ni njia rahisi ya kufanya wewe uwe na utele...
 
Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,915
Reaction score
4,062
Points
2,100
Nawasalimia wote kwa jina la Yesu.
Jana tulijifunza kuhusu kusamehe na kuachilia.

Moyo wa mwanadamu uliumbiwa upendo wala sio kubeba machungu, kinyongo, hasira, n.k

Ukipokea taarifa mbaya, au za kuudhunisha, au kukatisha tamaa usizipe nafasi wewe ziachie, fanya kama umetua mzigo, ukikaa nao utakulemea, utaongea mwenyewe road, utapata presha, utapata mawazo, mwisho ufe.

Kama unavyo kula na kunywa na baadae kushusha mzigo chooni, ndio ufanye hivo ili usaidie moyo wako usibebe vitu visivyo stahili kwa muda, mbona usipoenda haja(kubwa na ndogo) siku tatu utaanza kujiuliza na kuanza kutafta dawa.

Mbona moyo wako umeuacha na uchafu wa mda mrefu lakini ushtuki? Unajipenda kweli?

Mithali : Mlango 19

11 Busara ya mtu huiahirisha hasira yake;Nayo ni fahari yake kusamehe makosa.
 
Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,915
Reaction score
4,062
Points
2,100
Mwanzo 28:16-17
Yakobo alipoamka kutoka usingizini, akawaza, “Hakika Bwana yuko mahali hapa, wala mimi sikujua.” Kwa hiyo akaogopa, akasema, “Mahali hapa panatisha kama nini! Bila shaka hapa ndipo nyumba ya Mungu ilipo, hili ni lango la mbinguni.”

Tumejifunza kuhusu kutambua uwepo wa Mungu upo kila mahali, anaweza kujidhirisha hapa na pale hasijidhihirishe ila haiondoi ukweli kuwa yuko kila mahali, kwahvo katika shughuli zetu tutambue yakuwa yupo hapo, tufanye mambo yetu tukijua yuko kila mahali
kuna watu ni watakatifu wakiwa kanisani ila wakiwa nyumban, mtaan, sokon,kazin, kwenye gari n.k . wanakua watu hatari mdomo mchafu,maneno machafu, matendo nayo machafu.
 
Hakimu

Immortal Hero
KF Founder
Joined
Jun 3, 2023
Messages
2,821
Reaction score
6,503

Kweli kabisa
 
Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,915
Reaction score
4,062
Points
2,100
Bwana Yesu Asifiwe wapendwa..
Neno la leo church kwetu.

Ayubu 22:21
Mjue sana Mungu ili uwe na amani,
ndipo mema yatakapokujia.

Watu wengi wametafuta kuwa na amani na wamekuwa wakiitafuta amani pahala ambapo si sahihi.....
Wengi wamekua wakitaka amani wanakimbilia bar, pub, disco, club, kucheki mpira, n.k ila kiukweli amani ya kweli inapatikana Kwa Yesu.

Yeye ni mfalme wa amani na amesema amani anayo tupatia sio kama ya ulimwengu huu ambayo haidumu, ambayo inawalakini, inachosha, inagarana, na inaubaguzi..

Yeye akikuweka huru unakua huru kweli kweli.

Anza leo kumtafuta Mungu ili upate amani kutoka kwake....
 
Hakimu

Immortal Hero
KF Founder
Joined
Jun 3, 2023
Messages
2,821
Reaction score
6,503
Points
2,100
Neno la leo ni Kumjua Mungu tunayemtumikia, yaji sifa za Mungu wetu ilitusije fanya yasio mpendeza

1.Mtakatifu hivyo na sisi inabidi kuwa watakatifu
2.Habadiliki hivyo sisi tukiishika njia ya wokovu haitupasi kuwa ndani nje nje ndani
3.Mwenye haki hivyo na sisi inatupasa kuwa wenye haki
 
Hakimu

Immortal Hero
KF Founder
Joined
Jun 3, 2023
Messages
2,821
Reaction score
6,503
Points
2,100
Somo la leo kila mwokozi akizaliwa lazima apitie majaribu

Hivyo ukiwa unapitia magumu sana jua wewe umeletwa kwa kusudi flani chukulia mfano Musa, Samsoni na BWANA wetu YESU kristo aliye Mungu wetu
 
Kondeni0112

KF President
Platinum Villager
Joined
Jul 3, 2023
Messages
1,915
Reaction score
4,062
Points
2,100
Somo la leo kila mwokozi akizaliwa lazima apitie majaribu

Hivyo ukiwa unapitia magumu sana jua wewe umeletwa kwa kusudi flani chukulia mfano Musa, Samsoni na BWANA wetu YESU kristo aliye Mungu wetu
Thanks,
 
Similar threads

Huu ni uzi maalumu kwa ajili ya kuwatoa udenda au kuwatamanisha wana kijiji. Embe na Kichumvi kwa mbali😋😋
Replies
17
Views
724
Wanaume !! Kila mwenye jinsia ya kiume anaweza kuwa mwanaume, lakini sio wote wenye uwezo wa kuwa wanaume wanaostahili kuitwa wanaume. Je sifa za mwanaume ni hizi? Wanaume halisi ni sugu; hawapaswi kulia? Mwanaume hatakiwi kula chips mayai? Wanaume halisi hawakubali yeyote awaongoze? Wanaume ni...
Replies
44
Views
932
Oya weee leo tumention misemo iliyowahi kutamba sana mitaani Kula chuma hicho Apeche alolo Shega
Replies
48
Views
1K
Wasalaam Binafsi mimi sipo kwenye kundi lolote bado. Ila ningependa kuwa kwenye kundi la vegetarians hapo baadae. Hapa tunatupia recipes za vegans au vegetarians ili tuwe na range kubwa ya vyakula. Vegetarians- Hawa hawatumii nyama wala samaki kwenye milo yao au bidhaa au vyakula vilivyopikwa...
Replies
45
Views
961
  • Sticky
Wasalaam Huu uzi wa kipekee wa kutupia picha ya chakula unachokula. Sio lazima Updike wewe unaweza kuwa umenunua au umekipika. Ingependeza ukatupia picha ukiwa hujala na baada ya kula😀 NB: Usi upload picha ya chakula vinavyowekwa mtandaoni
Replies
663
Views
16K
Back
Top Bottom