Msaada wa Princess kifo na maisha ya ajabu na dada wa beach 🏖

Welcome to our community

Looks like you don't have an account yet? Be apart of something great, join today! Create account to get more access like posting, reacting to others helpful post and your own private message Register Or Login

Sehemu ya 1

Mapambano ya naanza ni siku nyingine Naitwa Thaibu kijana mchapa kazi, nilizaliwa mnamo tarehe 08/06/2004 nilimaliza elimu yangu ya msingi 2016 na siku bahatika kuendelea na shule

hivyo nilitumia mwaka mzima nyumbani mpaka pale nilipoona kuwa sasa inabidi niyajenge maisha yangu

Nilienda kwa baba yangu ambaye aliishi boko bunju, baba yangu huyu alishaachana na mama yangu Nia y kwenda ni kuomba mtaji wa biashara

Niliamini kuwa hapo ndipo nitakapo pata kila hitaji kwani alikuwa na maisha mazuri gari na nyumba kubwa, ila niliwaza kwanini alimtelekeza mama yangu katika nyumba ndogo na kwenda kuoa mwanamke mwingine?

Hayanihusu nilijijibu mwenyewe kwani sikuwepo kipindi cha ugomvi wao wala sikuwa najielewa

nilizungumza na mama kuhusu jambo hili, alipinga alipinga alipinga sana hakutaka hata kuaikia jina la huyo baba yangu

Nilitoka kwa hasira na kwenda chumbani kwangu nikiwaza ni kwanini? kwanini mama hataki kusikia jina la baba yangu ni kwanini?

nilijishauri sana kisha nikapitisha wazo hili kwakua ninamiliki simu ndogo na namba yake ninayo nitampigia na kumwambia kuwa nataka kuonana naye, historia fupi na huyu baba yangu ambaye sikuwahi kuongea naye kwa muda mrefu kutokana na kutokuwa na simu pia mama alinibana sana kwenye jambo hili alipinga na kupinga na kupinga na kupinga

siku moja baada ya mama yangu kunipatia simu ambayo alikuwa anatumia baada ya yeye kununja simu janja aliomba nimuhamishie namba zake zote na nifute kisha nibaki na simu hiyo, wakati nahamisha nilikuwa namtajia ambayo hakuitaka angesema na ningeifuta

ilipofika wasaa wa namba ya baba aliniangalia sana (aliisave kwa majina yote matatu) akasema ihamishe na ufute, nilihamisha ila sikufuta kwangu ndio sababu mpaka leo ninayo

Nilinyanyuka na kwenda kuchukua kibubu changu nilikivunja na kukusanya pesa zote ambazo nilifikia Tsh 50,000 zikiwa ni sarafu za miambili, nikachukua 1000 na kwenda kununua vocha nimpigie baba yangu

griiiiiiiigriiiiiiiigriiiiiiiiiigriiiiiiiigriiiiiiiigriiiiiiigriiiiii simu yake iliita na muda kidogo ilipokelewa

Baba: Haloo

Mimi: Shikamoo

Baba: Marakhaba nani mwenzangu?

Mimi: Nimimi Thaibu

Baba: Aaaa hujambo?

Mimi: Sijambo

Baba: Haya niambie

Mimi: Nataka kuonana na wewe ila usimwambie mama

Baba: Lini?

Mimi: Siku utakayo kuwa free

Baba: Njoo siku ya jumapili Jangwani sea breeze

Mimi: Ndo wapi?

Baba: Wewe njoo mpaka africana kisha nitakupitia

Mimi: Sawa

Baba: (Alikata simu haraka sana)

Ilikuwa siku ya Jumatatu hivyo nilikuwa na siku kadhaaa mbele kingine ambacho kiliniumiza kichwa ni kuwa nilishindwa kuelewana nae muda anyway nilijisemea ngoja niendezangu kijiweni karibu na stand ya daladala

Nilitoka zangu mdogo mdogo mpaka kijiweni oya vipi furesh furesh, sikieni wanangu wanangu mimi ninachange change nyingi (nikimaanisha sarafu za miambili) je wapi nitabadilisha kwa faida?

Mwanangu upo na mali na umekaa kizembe sikia sasa unaona hapo anza biashara ya kuuza change mbona inalipa, meza hii hapo ya mwana mbona hana tabu jamaaa maana alikula mtaji wote

Mimi: Bonge la wazo ngoja nikchukue pesa, wala sikungojea jua lizame nilitoka moja kwa moja mpaka nyumbani na kubeba elfu 30 kwenye mfuko na kuja nazo stand na kuzipanga

nilijiongeza kwa kusema kuwa kwenye buku mbili nakata 200 tu

Niliuza sana change japo hazikuisha na siku iliyofuata pia niliuza na pesa ikawa imeisha yote ni noti, nikazitunza pesa zangu na sikuendelea na biashara hiyo kwani mma aliikataaa katakata na kusema kuwa inakudhalilisha sana

kesho yake ahsubuh nilikwenda tena kijiweni katia story za hapa na pale ndio rafiki yangu mmoja alisema unajua biashara ya kuuza bangi inatoa sana, nilitege masikio yangu niisikilize vizuri kwani jamaa katika kijiwe ndio don pale, yan ukiuza kilo zako kadhaa tayariii umetoboa

Oya wewe usitake kutuchomesha tumeridhika na umasikini wetu kubet kutatutoa siku moja, Ok sawa jamaa alijibu na kuendelea story nyingine,

Huyu Mbwa anapesa kumbe sababu ya bangi hapo nikipiga kipengele kimoja napata pesa nakula nachomokea zangu kushoto "Nilijiwazia hivyo"

Wiki ilikatika sana mpaka jumapili ambapo nilivaa nguo zangu vizuri na kuanza safari mida ya saa moja ahsubuh, mkuu mosi mguu pili kwenye daladala na kushuka hapo mbezi beach afrikana, ilitimia saa 3 ahsubuh nilipiga simu ya baba akapokea na kusema Nisubiri nakuja kisha akakata simu

Ndugu tutafute pesa tu maana nilikaa mpaka saa tisa na nusu jioni ndio mzee kaingia na RangeRover, Dogo panda twende

Tuliondoka mimi na babu mpaka beach moja tukatafuta sehemu ambayo ilikuwa imetulia, akaagiza chakula sikutaka kuremba wala nini nilianza kugonga msosi

Baba: Kijana taratibu, unashida gani?

Mimi: Nilifeli darasa la saba ninaomba mtaji wa biashara

Baba: Hivi unajua baba yako alishafariki mimi sio baba yako, nivile tu unatumia jina langu, nimependa kujitoa kwako nitakupa mtaji kiasi ilinufanye biashara ila huo ndio msaada wa mwisho kwako, nitakupigia, aliniachika 50,000 na kuondoka

Chakula kilinishinda kwani sikutegemea kusikia kuwa yeye sio baba yangu

ITAENDELEA...
 

AlmightyGod

Active Villager
Joined
Jun 4, 2023
Messages
464
Reaction score
1,335
Points
1,900
Sehemu ya 2

Hata hivyo sikuvuta sana niliamua kwenda zangu baharini na kutulia hapo, griiiiii ni mama anapiga
Mama: Haloo upo wapi?
Mimi: Nipo beach mama
Mama: Ukija utakuta ufunguo kwenye jiwe mimi nasepa sehemu narudi kesho
Mimi: Sawa

Hahhaha leo mbuzi kaachiwa, nilisema hivyo kwakua nilitaka nisambaeeee sana hapo nikicheki huku na huku
Habariiii, Nilisikia sauti nyororo ya kike huku akikaa karibu yangu
Poa, Nilijibu
Mbona umepooza nilikuona tangu kitambo,
Nipo tu, Nilijibu
unaitwa nani,
Thaibu, nilijibu
Unasimu?
Mimi: Sinaaaa
sasa wewe kijna mzuri kabisa unakosa simu?
Mimi: Ndio simu sina ila ninamawasiliano
hahahahahahahahh ndio hayo ulioshika?
Mimi: eee ndio
Twende ukachukue simu ninayo nimeacha nyumani kwani siwezi kutumia simu mbili
Mimi: sawa

Kweli nilimfuata kwa nyuma nisijue tunakwenda wapi, sifa ya mwanamke huyu ni kuwa alikuwa mrefu kiasi, mwili wa wastani, trakkkk kdg na maziwa ya wastani ila kwa muonekano alikuwa namba B yani umri umesogea kidogo,
Baada ya miguu kadhaaa tulitokea parking ambapo toyota juke ilipaki mwanzoni, aliingia na kuniambia twende unaogopa?

Mimi: Hapana, huku nikifungua mlango na kuketi ndani ya gari, tunakwenda wapi?
Tunakwenda nyumbani Osterbay
Mimi: sawa
Kimya kilitawala kwa muda fulani kisha akasema unaumro gani?
Mimi:12 years
Elimu yako?
Mimi: Nimefeli darasa la saba
Mbona umemaliza shule mdogo sana?
Mimi: Ndio
Nataka kuishi na wewe maana unaonekana unakili sana
Mimi: Mama yangu amenitupa sana, na kisa cha kufeli shule ni kwa sababu baadhi ya siku za mitihani sikuwepo mama alinitaka niende mahali ambapo alifanyia biashara
Nimekumbuka jambo...
Mimi: Jambo gani?
Kwanini huku niamkia
Mimi: Shikamooo nilisahau kidogo (ila kiukweli haukuwa tabia yangu kwani story za vijiwe vilinifaya kuona wanawake kama sehemu ya starehe)
Markhaba tumefika

waooo ni bonge la jumba alifungua mlango na kutaka niingie ndani, niliketi kwenye kochi nikisubiri nini kitafuata, alikuja na simu nisijue ni aina gani ila ilionekana brand new sana, haya hii simu nakupa ila inalaini tayari hivyo wewe hamisha majina yako tu
Mimi: Hapana mimi ninayo laini
Ok basi weka, ila mimi nitakutafuta kwenye laini yangu hii tu only for emergency nitatumia laini yako
Mimi: Sawa
Nenda ukaoge, taulo na kila kitu kipo huko bafuni mlango ule pale ndani
Mimi: Aaa sina jasho sana nielekeze njia niende nyumbani,
Watoto wazuri sio wabishi Aya nenda

Nilinyanyuka mguu mosi mguu pili mpaka kwenye chumba, chumba kilikuwa kizuri sana kitanda kikubwa, mashuka meupe, kabati na tv nilizama moja kwa moja mpaka bafuni na kuvua nguo zangu, nikaoga vizuri kisha nikajifuta na kuvaa tena nguo zangu

ila natoka tu bafuni Namwona yule dada kaka kitandani, nikajiwazia kwaiyo ningevulia nguo hapa angenichungulia mdudu wangu

Alisema chukua hii perfume, alafu ulisema unaishi na mama yako nipe niongee naye ili nikurudishe kesho wakati naenda kazini, sikupinga jambo lile sababu nilitaka nilale kwenye jumba na kifahari sana, nikampatia simu ikiwa napiga simu ya mama yangu lakini kila ikipigwa ni namba unayopiga haipatikani

Mhhh huyu mama yako hatari haya panda tulale,
kwani hiki ni chumba chako? Niliuliza
Hapana ninakupa kampani tu mgeni, huku akitabasamu
Aliiwasha tv tukicheki tom and Jerry no stress tukicheka, nilisahau kabisa mambo ambayo baba yangu aliniambia kuhusu mimi

Prince amka, ilikua sauti ya yule dada, cha kwanza nilitazama tv nikakuta imezimwa,
Ni ahsubuh chukua mswaki dawa ipo bafuni uende uoge unywe chai tuondoke
Shikamooo, Marakhaba prince, nilinyanyuka nikajisafisha kwa kuoga na kuswaki kisha nikajifuta maji na kurudi chumbani

twende nilisikia sauti ya mwanamke mwingine ambaye alionekana mfanya kazi tu kwa muonekano wake
Nilimfuata nyuma nyuma mpaka sitting room, nikapewa kikombe cha chai ya maziwa, mikate yenye jam ya chocolate na two boiled eggs
Nikaigonga chap kisha nikamuona dada akija na kusema tayri twende

tukapakiana kwenye usafiri wake kuelekea nyumbani nilimwambia ninapokaa na kusema aliwahi kufika mara mbili na hiyo nyumba anaijua
Mimi: ohhh kumbe je ungependa nikuite nani? hukuniambia jina lako,
Niite princess shani jina langu ni shani ila princess itapendeza
Mimi: aaaa princess alafu mzuri kama jina lako
princess: (alinikata jicho la kucheka, kushanganzwa na kupenda) kwani hakuamini kama ningesema hivyo
Mimi: Nilitingisha kichwa chini juu kuonesha kuwa yes ni kweli
Princess: Ahsante mwana mfalme wangu
Mimi: sawa

Tulifika nyumbani na nilimkuta mama akisimama getini akitizama huko na huko kama mtu mwenye wasiwasi tu wa kawaida
Thaibu kenge wewe ulikuwa wapi nimerudi nimerudi ahsubuh alafu inaonekana hukuwepo na chakula hukula
Mimi: samahani mama
Princess: shikamoo
Mama: Marakhaba
Princess: Nilikuwa naye mimi jana tulikupigia haukupatikana
Mama: Mlikuaa wapi?
Princess: Nyumbani kwangu, kama hutajali twende ndani tuongee mama yangu
Mama: Karibu sana
Princess: Mama mimi naomba nikae na mwanao nimpe elimu na kila kitu
Mama: Unashingapi???
Mimi: Mama unaniuza kwanini?
Mama: wewe siunajifanya mjanja sana ulikwenda kuongea na baba yako, alikwambia kuwa tulikuokota mimi nilishauharibu uzazi wangu kwa kutoa mimba kudanga ndio kunakulisha nimekuchoka sawa
Princess: Sio maneno mazuri kumwambi mtoto
Hapo machozi yalinitoka nisijue kwanini yananipita mama yangu kumbe nae ndio adui ananisema hivi
Mama:Eeee ndio hivyo kila siku anakula tu bure mpaka hapo alipo shukuru tu, nimechoka kulea yai na bao la wengine ambao hata kukulea wangeshindwa
Princess: Kwani ulimtoa wapi?
Mama: Miaka 11 nyuma nilikuwa na mahusiano na huyo anayedhani baba yake, siku moja baada ya baba huyo kugundua kuwa nimetoa mimba mara nyingi kwenye maisha yangu na nisingeweza kubeba mimba alinitukana sana na kuniita malaya
jioni yake bwana huyo alisema twende nikurudishe kwenu siwezi ishi na ww usiniletee nuksi mimi, nilikubali kwa moyo wote ila nyumbani walileta upingamizi sana hivyo tulirudi wote nyumbani na huyo mzee
baada ya siku kadhaa dada yake na huyo baba aliumwa sana hivyo tulienda wote kumwona lakini mungu alimpenda zaidi, siku ya mazishi yake wakati nimekaa na huyo bwana alikuja mama mmoja hivi na kunipa mtoto akisema nimshikie, kweli nilikubali moyo mmoja kwani ni kwa muda tu, tulikaa sana mama yule hakurejea hata ikabidi baba huyo atafute utaratibu wa kumtafuta baada ya kama simu mbili tulikuta mama yule kajinyonga na tusijue wapi kwa kupata ndugu zake kwani alikuwa mtu aliyepewa tu hifadhi kijijini hapo

jukumu la kulea hiki kiumbe kilikua yetu (kiumbe akimaanisha mimi) na mda kidogo tulitalakiana na yule bwana na alimkana mtoto kwenye matumizi yote, niliangaika ale ashibe iliakifika umri fani asepe kivyake ila toto lenyewe ndo hili huenda pesa nilizomlisha ningejenga hata heshima baa

kusema ukweli yale maneno yaliniuma sana sana kwani sikutegemea kuwa mama yangu angenichukulia hivi hata kwa dakuka moja

Mama: kwaiyo utanilipa sh ngap nikuachie uishi naye?
Princess: Akionekanakusononeka sana akasema 1M ila twende ustawi wa jamii tuandikishiane kbisa kwa kunikabidhi huyu kijana

KWELI baada ya muda kidogo tulitoka mimi na mama na princess mpaka ustawi waliandikishiana na mimi nililidhia kuondoka kwani nilishajenga chuki kubwa sana na mama na nilisema sitamtafuta yeye wala baba, nilimkabudhi laini yake na kufuta kila namba na tuliondoka na princess
tulienda shopping ya nguo nyingi na baadhi ya vitu pia alininunulia Mp4 memory card ambayo nilimuomba aninunulie

tofauti na jana siku hiyo wala sikuwa na furaha sana, hivyo tu ilibidi nioneshe meno kwa mdhamini tu

ITAENDELEA
 

Similar threads

Wakuu nipo alone mwenyewe huku muda umesonga kigiza kimeingia ila sijui nipike nini au ninunue kiepe? Wadau nipeni mawazo msosi wa chap ambao hautumii nguvu na ela nyingi duh nimekuwa mvivu wa kufikitia Gily Leejay Katkit
Replies
15
Views
555
Tatizo la kunyonyoka kwa nywele na kuwa na kipara limekuwa likiwatatiza wanaume wengi kwa muda. Shida hii mara nyingi huanza wanaume wakiwa wana miaka 30 hivi, na kufikia umri wa miaka 50 nusu ya wanaume huwa wanakabiliwa na tatizo hili. Tatizo hili hutokana na vinyweleo vya nywele, ambavyo...
Replies
18
Views
346
Ndugu zangu nazani mnajua ya kwamba mimi niko single, nmekuja hapa ili mnisaidie jambo hili... Kipindi cha nyuma kidogo nliangaliaga series ya GOT (game of throne).. kwa kweli nlijikuta nampenda sana huyu dada mother of dragon, Nasijawai penda mdada mwingine mpaka leo hii, kwahvo inanibidi...
Replies
49
Views
630
Oya wadau mwenye mbinu ya kunisaidia niweze kuongeza pesa zangu mara mbili au zaidi, yaani kudoubling hela nliyonayo sasa.. tupeane michongo
Replies
64
Views
1K
Wanakijiji amani ya Mungu iwe nanyi Naomba msaada kwa ajili ya mtoto huyu wa mjomba. Kwanza mjomba alizaa na mwanamke wa kichagaa wakaachana sababu sifahamu kwani nilikua mdogo kiasi. Sasa baadae mjomba akaja kuoa mwanamke mwingine wa kichaga ambae yupo bae mpaka sasa. Msaada ninao taka kutoka...
Replies
12
Views
318
Back
Top Bottom