- Jun 28, 2023
- 303
- 877
- 1,900
Wanakijiji amani ya Mungu iwe nanyi
Naomba msaada kwa ajili ya mtoto huyu wa mjomba. Kwanza mjomba alizaa na mwanamke wa kichagaa wakaachana sababu sifahamu kwani nilikua mdogo kiasi.
Sasa baadae mjomba akaja kuoa mwanamke mwingine wa kichaga ambae yupo bae mpaka sasa.
Msaada ninao taka kutoka kwa wachaga ni juu ya huyu mtoto ambae alizawi kisha wazazj wakaachana japoa hawakufunga ndoa.
Katika kutengana kwao mtoto alienda na mama ila baada ya miaka mitatu yule mama akaja akamuacha mtoto mlangoni mtoto akalelewa amemaliza form four mwaka jana.
Huyu mtoto sasa amekua na changamoto nyingi nyingi mara atake kujiua, mara azurure mtaani kama kichaa, mara aamke atukane ndugu upande wa baba kwa meseji tele, yani unaweza ukaamka na kukuta meseji 50 anakuambia mambo mengi yasiyoeleweka, mara anatuchukia, kiufupi haeleweki japo darasana anafanya vema.
( kuna kipindi hapo kati aliondoka kwa baba yake akaenda huko kwa wajomba zake wachaga)
Sasa huko alipo tukasikia mara alikamatwa na polisi anazurura wakamhoji mwisho wa siku wakamuachia. Baada ya tukio hili ndugu zake upande wa mama wakaja kwa mjomba hawakumkuta wakimtaka aridhie huyu mtoto akafanyiwe mila ili atulie hvyo kama ataridhia sijui anunue mbuzi wawili wakachinjwe kaburini kwa babu yake na mtoto kwani babu huyo hakupenda mtoto alivyoletwa kwa baba yake kipindi kiwa mdogo hvyo kukasirika kwake akasema maneno kua mtoto hatotulia maisha yake yote lazima awasumbue.
Sasa wachaga haya yanaweza yakawa na ukweli? Maana mtoto ana heka heka mpaka hatuelewi. Samahani kama nitakua sijaeleweka mie mzuri kuongea ila kuandika mtiti